24th September, 2018
Naibu wa Rais William Ruto hatiamaye amejiunga na mjadala unaoendelea kuhusu ushuru wa ziada akiunga mkono hatua ya rais uhuru kenyatta ya kutia saini sheria ya utekelezaji wa sheria hiyo iliyoongeza bei ya bidhaa za petroli kwa kiwango cha asilimia 8. Akizungumza katika kaunti ya nandi wakati wa uzinduzi wa mpango wa ajenda 4 kuu za serikali, ruto amedai kuwa ongezeko la gharama ya maisha limesababishwa na wafanyibiashara walafi ambao wametumia sheria hiyo kuongeza bei za bidhaa maradufu.