.
22nd September, 2018
Gavana wa Migori Okoth Obado kwa siku ya pili atakuwa kororoni hii leo katika kituo cha polisi cha Gigiri alikozuiliwa tangu jana.
OCPD wa kituo cha polisi Gigiri Richard Mwangi amesema kuwa Gavana wa Migori Okoth Obado yuko salama.
Hapo awali taarifa zilitanda kwenye mitandao ya kijamii kuwa Gavana Obado aliugua na kupelekwa hospitalini.
Obado alitiwa mbaroni hapo jana kuhusiana na kifo cha Sharon Otieno aliyeuwawa kinyama wiki mbili zilizopita.