18th September, 2018
Jukwaa la Wahariri limefanya mkutano ambao maudhui yalikuwa kutafuta mbionu ya kukomesha ongezeko la mashambulizi kwa Wanahabari nchini. Mkuu wa polisi Joseph Boinnet alikuwa mgeni mheshimiwa katika hafla hiyo na kuihakikishia jamii ya wanahabari kuwa hawatadhulumiwa wakiwa kazini. Kadhalika alivitaka vyombo vya habari kujiepusha tu kuandika ama kuwasilisha habari ambazo alizitaja kuwa mbaya.