.
15th September, 2018
Menengai Cream Homeboyz, Mwamba RFC, Uganda Emerging Sevens na Mean Machine wametinga robo fainali ya raundi ya mwisho ya msururu wa raga nchini Christie Sevens, baada ya kushinda mechi za makundi.
Homeboyz ilifuzu robo fainali baada ya kuwalaza mabingwa wa Driftwoods Sevens Nakuru Top Fry alama 43 kwa12, huku mabingwa wa Dala Sevens Mwamba RFC wanaoshikilia nafasi ya pili katika msururu wa raga nchini wakiwashinda Kabras Sugar 31 21.