Wanawake wamefanya maandamano wakikashifu mauaji ya Sharon Otieno

KTN News Sep 11,2018


View More on KTN Leo

Wanawake kutoka matabaka mbalimbali leo hii wamefanya maandamano ya amani katikati mwa jiji la nairobi wakikashifu mauaji ya mwanafunzi wa chuo kikuu cha rongo Sharon Otieno. Wakiongozwa na vuguvugu la kutetea haki za binadamu Coalition for grassroot sawa na baadhi ya wawakilishi wa vyuo vikuu, wanawake hao wametaka kutwaliwa kwa vyeti vya kusafiri vya washukiwa wote wa mauaji hayo. Wakikariri historia ya visa vya mauaji ya wanafunzi wa vyuo vikuu ambavyo hutekelezwa na watu mashuhuri pasi na kuchukuliwa hatua yoyote. Wanataka vyombo husika kuharakisha shughuli ya uchunguzi.