10th September, 2018
Gavana wa Nairobi Mike Sonko amesema hajahusika kwa njia yoyote kwa yale masaibu yanayomkumba spika wa kaunti ya Nairobi Beatrice Elachi. Amesema pia viongozi wa kaunti wanaweza kutolewa ofisini, pindi tu wawakilishi wa wadi wanapokuwa na tashwishi na uongozi wao.