1st September, 2018
Ni rasmi kwamba wakenya wataanza kushuhudia hali ngumu ya maisha. Hii ni baada ya sheria mpya ya kutoza ushuru wa ziada, almaarufu vat kwenye bidhaa za mafuta jinsi alivyoagiza waziri wa fedha, henry rotich. Uchunguzi wa ktn umebaini kwamba wahudumu wa magari ya abiria wameongeza nauli kwa kati ya shilingi mia mbili na mia tatu kwa abiria wanaosafiri kutoka nairobi hadi maeneo ya mombasa, kisumu, meru na kakamega.