.
1st September, 2018
Katibu Mkuu wa Muungano wa Vyama vya Wafanyikazi nchini COTU, Francis Atwoli amemuomba Rais Uhuru Kenyatta kusikia lalama za Wakenya kwa kutia sahihi mswada wa bunge, unaositisha kupanda kwa ushuru wa mafuta humu nchini. Atwoli amemlaumu waziri wa fedha Henry Rotich kwa kukiuka matakwa ya bunge na kupandisha bei ya mafuta, hali iliyopandisha gharama ya maisha kwa asilimia ishirini. Alikuwa akizungumza na wanahabari nyumbani kwake huko kajiado.