Washukiwa wa sakata ya mahindi wafikishwa mahakamani

KTN News Aug 30,2018


View More on KTN Leo

Washukiwa wa sakata ya mahindi akiwemo katibu wa kudumu wa wizara ya kilimo Richard Lesiyampe wamefikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya matumizi mabaya ya mamlaka, ulaghai na utumizi wa fedha za umma bila idhini. 

Jumla ya watu kumi na sita wanasakwa na tume ya EACC kwa kuwezesha wakulima bandia kujipatia bilioni 1.9 huku wakulima halisi wakiangua kilio.