Wanajeshi watano wa KDF wauwawa kwenye msafara

KTN News Aug 29,2018


View More on KTN Leo

Wanajeshi watano wa KDF wamefariki huku 10 wakiendelea kupokea matibabu, baada ya lori lao kukanyaga kilipuzi cha kutegegwa ardhini huko kiunga kaskazini mwa pwani ya kenya.
 
Shambulizi hilo lilitokea kwenye  barabara kuu ya kuelekea Kiunga kutoka sehemu ya Sankuri mwendo wa saa mbili asubuhi. 
 
Wanajeshi hao wa KDF walikua wakielekea vijiji vya kiunga katika msitu wa Boni kupeana misaada ya maji na vyakula kwa wakaazi hao.
 
 Msemaji wa jeshi la KDF Paul Njuguna aliwashukuru wenyeji kwa ushirikiano wao baada ya tukio hilo.