Martha Karua: Ipo haja ya kubuni sheria za kudhibiti kampeni nchini

KTN News Aug 28,2018


View More on KTN Leo

Kiongozi wa NARC Kenya Martha Karua amesema ipo haja ya kubuni sheria za kudhibiti kampeni nchini. Karua ameikosoa bunge kwa kutotekeleza mswada uliopitishwa wa kudhibiti ufadhili wa fedha za kampeni. Kinara huyo wa chama cha narc kenya ameonya iwapo mswada huo hautatiliwa maanani basi kampeni zitakuwa ni za wale wenye fedha tu. . Karua amesema ni sharti sheria ya kuchunguza matumizi na mbinu za kupokea fedha za kampeni itiliwe mkazo, kwani ufisadi na wizi wa fedha za umma hutekelezwa zaidi wakati wa kampeni. Aliyasema haya kwenye kongamano la centre for multi?party for democracy hapa jijini Nairobi.