27th August, 2018
Huku taifa likiadhimisha miaka minane tangu kuzinduliwa kwa katiba, mwaka wa 2010, sasa minong'ono imeibuka kutoka bungeni ambako yadaiwa huenda bunge la senet linajivunia madaraka bandia. Licha ya kuwa na afisi za kiongozi wa walio wengi na walio wachache, afisi hizo hazitambuliwi kwenye katiba. Ukweli wa mambo ni kwamba kifungu cha 108 cha katiba kinatambua afisi za kiongozi wa wengi na walio wachache katika bunge la taifa pekee. Je, wanaoshikilia afisi kwenye seneti hadi sasa wanayo madaraka bandia? Mwandishi wetu wa masuala ya siasa duncan khaemba amelizamia swala hili na anatupa taarifa hiyo kwenye awamu ya kwanza la makala maalum, state of the constitution.