Hassan Joho ameushinikiza wito wa ukaguzi wa hali ya kimaisha

KTN News Aug 27,2018


View More on KTN Leo

Matamshi ya Gavana Ali Joho yamekashifiwa vikali na baadhi ya viongozi wa eneo la bonde la ufa, wakidai joho hafai kuzungumza kama msemaji wa bonde la ufa na badala yake anafaa kushughulikia maendeleo ya eneo la pwani. Wakiongozwa na mbunge wa kapseret oscar sudi kwenye kikao na wanahabari mjini eldoret,viongozi hao wamedai tume ya maadili na kupambana na ufisadi eacc inatumiwa na wanasiasa fulani katika kuwahujumu wapinzani wao kwa lengo la kuyumbisha ndoto zao za kuwania uongozi mwaka wa 2022.