Wamemavyo Waganda:Wafuasi wa Bobi Wine wateta

KTN News Aug 20,2018


View More on KTN Leo

 
Viongozi wa upinzani nchini Uganda wameshikilia kwamba 
wabunge wa upinzani wamekamatwa, kunyanyaswa  na kuzuiliwa na vyombo vya dola nchini humo. 
Hii ni baada ya taarifa kusambaa kwenye mitandao ya kijamii, 
ikionyesha mmoja wa wabunge hao akiwa katika hali 
mbaya. Miongoni mwao ni Robert Kyagulanyi, mbunge na 
msanii maarufu nchini humo kwa jina jingine Bobi Wine. Bobi 
Wine amekuwa maarufu tangu kuingia bungeni mwaka 
uliopita, na semi zake za kuushambulia uongozi wa rais 
Yoweri Museveni zimepokelewa kwa shangwe muda wote na 
wananchi waliochoshwa na uongozi wa serikali ya Museveni. 
polisi nchini humo wanaarifu kwamba Bobi Wine na Francis 
Zaake walikamatwa baada ya wafuasi wa mgombeaji mmoja
  huru kurusha mawe kwa msafara wa rais Museveni,
siku ya juma tatu katika eneo la West Nile