Vurumai Mazishini: Kisa chatokea Trans Nzoia,Polisi wawajeruhi waombolezaji
20th August, 2018
Watu wanne wakiwemo mwakilishi wadi wa Kapomboi Kaunti
Trans Nzoia Benard Wanjala na Walinzi Wawili wa wabunge
wa Tongaren na Likuyani wamejeruhiwa vibaya kwa risasi
baada ya vurugu kuzuka kwenye matanga ya aliyekuwa
dereva wa mbunge wa Lukuyani Enoch Kibunguchy aliyeuawa
kwa kupigwa risasi juma moja lililopita.
Akikashifu kitendo hicho kilichotokea baada ya mmoja wa mawaziri
wa kaunti ya Kakamega kuwasili mahali hapo, Seneta wa
Bungoma Moses Wetangula amemtaka kamishna wa polisi na
kiongozi wa mashtaka ya umma kuagiza uchunguzi ufanywe
na kumshtaki afisa huyo wa polisi ambaye alifyatua risasi
kiholela kwenye umati. Mazishi hayo yalikuwa
yamehudhuriwa na viongozi wa FORD Kenya kutoka eneo la
Magharibi. Majeruhi walipelekwa kwenye hospitali ya binafsi
ya kiminini cottage na hospitali ya mt. Elgon mjini Kitale