19th August, 2018
Kinara wa NASA Raila Odinga amesema ana imani kwa kamati ya uwiano kutekeleza maafikiano kati yake na rais Uhuru Kenyatta.
Wawili hao waliafikia kuweka tofauti zao za siasa kando ili kuwaleta Wakenya wakibuni kamati ya watu kumi na tano kuangazia maafikiano yao.
Baadhi ya vigezo vya maafikiano hayo vikiwemo kukabiliana na ufisadi na suala ukabila. Raila alizungumza alipohudhuria ibada katika kanisa la friends church quarkers kitongoji cha maringo hapa jijini Nairobi.