16th August, 2018
Mmiliki wa jumba la biashara la Air Gate center, awali likifahamika kama Taj Mall, Ramesh Chandria, sasa ameitaka serikali kuendelea na mpango wa kulibomoa jengo hilo, ila kwa onyo kwamba ubomaoji wa jumba hilo utaishia yeye kufidiwa mabilioni ya fedha.
Akizungumza na wanahabari kufuatia ilani ya wiki mbili ya ubomoaji, Ramesh ameshangaa ni vipi wawekezaji ndio wanaolengwa na ilihali mijengo yote iliidhinishwa na serikali.