.
13th August, 2018
Mwenyekiti wa tume ya ardhi nchini, Muhammad Swazuri na mkurugenzi wa shirika la reli nchini, Atanas Maina, wamefikishwa mahakamani pamoja na wengine 12 na kuyakana mashtaka ya ufisadi dhidi yao. Wakuu hao wanatuhumiwa kuipunja serikali jumla ya shilingi milioni 221.3 kabla ya kuachiliwa kwa dhamana.