×
× KTN KTN News KTN Morning Express KTN Leo Leo Mashinani The Big Story Checkpoint News Center E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian Entertainment Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified Jobs Games Crosswords Sudoku The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login
×
Show Swahili

Vijana wawili wafariki Embu baada ya kutumbukia mtoni

6th August, 2018

Vijana wawili wa umri wa miaka 14 na 17 wamekufa maji katika kijiji cha Ngomano viungani mwa mji wa Embu. Vifo vya wawili hao vilithibitishwa baada ya nguo zao na baiskeli waliokuwa wakitumia kupatikana katika kingo za mto Rupingazi. Inadaiwa kwamba Alex Mwenda na Emmanuel Murimi ambao ni wanafunzi wa darasa la nane na kidato cha tatu mtawalia, waliondoka nyumba kuelekea matembezi baada ya kuhudhuria ibada ya jumapili ila hawakuonekana tena.inakisiwa kuwa huenda walielekea mtoni kuogelea. Juhudi za kuwasaka zilianza walipochelewa kufika nyumbani.akithibitisha kisa hicho. Naibu wa chifu wa eneo la kamiu samuel njagi amesema juhudi za kuwasaka wawili hao hazijazaa matunda.amesema wamewasiliana na wapiga mbizi ili wasaidie katika kusaka miili ya wawili hao.

.
RELATED VIDEOS