30th July, 2018
Kwa muda mrefu mboga za kienyeji zimechukuliwa kuwa kitoweo cha watu waishio vijijini na wala sio mijini. Lakini baada utafiti kubaini kwamba ulaji wa mboga za kienyeji una manufaa ya afya mwilini kukiwemo kudhibiti maradhi kama vile saratani na uzani kupita kiasi, upanzi na ulaji wa mboga hizo umeanza kupata umaarufu. Katika eneo la magharibi ya Kenya, baadhi ya shule zimezifanya mboga za kienyeji kuwa kitoweo cha msingi katika lishe kwa wanafunzi.