29th July, 2018
Gavana wa Kaunti ya Kilifi Amason Kingi sasa anaitaka serikali ya kitaifa kuchapisha ripoti ya tume ya ukweli haki na maridhiano ikiwa imejitolea kumaliza dhuluma za kihistoria humu nchini. Kingi amesema kuwa salamu za heri sasa zinapaswa kutoa fursa ya kushughulikia tatizo la ardhi linalowakabili wenyeji wa kaunti ya Kilifi.