.
18th July, 2018
Kulikuwa na kizaazaa katika maziara ya mji wa Nakuru pale wakazi walipovamia na kusimamisha mazishi ya mtoto wa umri wa miaka 14 anayedaiwa kufariki baada ya wazazi wake kupuuza kumpeleka hospitalini . Wakazi wanadai kwamba familia hiyo inafuata dini yao ya kutoruhusu wagonjwa kutibiwa hali ambayo imesababisha vifo vya watoto 7 kufikia sasa.