Wanawake wa KANU waunga mkono juhudi za rais katika vita dhidi ya ufisadi

KTN News Jun 28,2018


View More on KTN Leo

Kongamano la taifa la wanawake wa chama cha KANU, limeunga mkono juhudi zinazoendeshwa dhidi ya ufisadi na kukariri haja ya viongozi wote kumwunga mkono rais Uhuru Kenyatta katika harakati hizo. wakiongozwa na mwenyekiti wa taifa wa kina mama chamani humo, Elizabeth Kimkung’, viongozi hao wa kike aidha waliwakashifu wale wanoendesha siasa za 2022 na badala yake kuwataka wazingatie utendakazi kazi badala ya siasa.