.
21st June, 2018
Thika Queens wameendeleza matumaini yao ya kuponyoka na taji la ligi kuu ya kina dada nchini kwa kuwatitiga Spedag mabao manne bila jibu
Mshambuliaji wa Harambee Starlets Mwanahalima Dogo Adam alifunga mabao mawili kwa mpigo nao mercy achieng na christine kitaru wakaongeza moja kila mmoja kuwapa malkia hao alama tatu muhimu. kufuatia ushindi huo, Thika Queens wamezidisha uongozi wao kileleni mwa jedwali hadi alama 39 baada ya mechi 13.