Mswada wa kuwaondoa mawaziri wazua mgogoro bunge Kisumu

KTN Leo | Wednesday 13 Jun 2018 9:08 pm

Mswada unaolenga kuwaondoa mawaziri wawili katika serikali ya kaunti ya Kisumu umeibua hisia mseto na kuzua mgogoro mkubwa katika bunge la kaunti hiyo.  Baadhi ya wawakilishi wadi wanasema mswada huo haufai kujadiliwa kwa sasa huku wengine wakitaka ujadiliwe. Inaelekea bunge la kaunti hiyo linabuni mbinu ya kuwapatanisha waakilishi hao kwa kuwapeleka katika ziara ya mafunzo nchini Rwanda.