.
28th May, 2018
Kiungo muhimu wa timu ya Wazito Pistone Mutamba alimpa kocha mpya wa timu ya taifa Harambee Stars Sebastian Migne ushindi wake wa kwanza tangia kutwaa mikoba ya uongozi wa timu ya taifa. Pistone Mutamba alipachika bao hilo la pekee kunako dakika ya 74 baada ya bao hilo kuzalishwa na Ovella Ochieng huku Kenya ikimiliki asilimia kubwa ya umisili.