6th May, 2018
Muungano wa wafanyikazi wa kilimo umepaaza hisia zake kutoka na tishio la maisha ya katibu mkuu wa muungano wa wafanyikazi nchini Francis Atwoli. Wakizungumza mjini nakuru, viongozi wa muungano huo wamewaonya wanaopanga hila dhidi ya atwoli kuwaacha kwani mamilioni ya wafanyikazi nchini wanamuunga mkono huku wakitoa wito kwa vyombo vya usalama kumpa usalama wa kutosha na kuharakisha uchunguzi wao.