5th May, 2018
Mbunge wa baringo kusini Grace Kipchoim amezikwa nyumbani kwake eneo la Mochongoi kaunti ya Baringo. Viongozi mbali mbali akiwemo naibu rais william ruto na seneta wa Baringo Gideon Moi walihudhuria na kumsifu Bi kichoim kwa kujitolea kwake kuhudumia waliochagua licha ya changamoto za kuuguza saratani japo siasa za rift valley pia zilijitokeza.