.
24th April, 2018
Rais Uhuru Kenyatta ameahidi kuendelea kuunga mkono ugatuzi huku akionya kuwa serikali yake itakabiliana na maafisa wanaopanga kuiba pesa za umma. Rais Uhuru aliyekosa kuhudhuria kongamano hilo mjini Kakamega na badala yake kutoa hotuba moja kwa moja kutoka Ikulu amesema ajenda yake ya masuala manne makuu itafanikiwa iwapo hakutakuwa na siasa nyingi au ufisadi.