5th April, 2018
Mahakama kuu imeamrisha kesi inayomhusu Philip Onyancha aliyewahi kukiri kuwaua watu 18 na kufyonza damu yao kuanza upya. Wakati huo huo, afisa wa polisi Titus Ngamau anayefahamika maarufu kama katitu ambaye kuzuiliwa kwake kulizua maandamano makubwa mtaani Githurai amehukumiwa miaka 15 gerezani kwa kosa la mauaji.