12th March, 2018
Hatma ya muungano wa NASA iko mikononi mwa vyama tanzu vya muungano huo. Hii ni baada ya vinara wote wanne waliokutana mjini Athi River hii leo kuafikia kuwa vyama tanzu ndivyo vitaangazia mustakabali wao baada ya muafaka wa mwishoni mwa juma lililopita kati ya Rais Uhuru Kenyatta na Raila Odinga.