.
8th March, 2018
Timu ya taifa ya kabaddi inaendelea na matayarisho ya mashindano ya kufuzu kombe la dunia yatakayoandaliwa nchini Tanzania mwezi huu. Huu utakuwa mkondo wa pili baada ya mkondo wa kwanza uliofanyika nchini Rwanda mwaka jana ambapo Kenya ilishinda medali ya dhahabu.