6th March, 2018
Waziri wa afya Sicily Kariuki ameendelea kujipata mashakani kufuatia hatua yake ya kumsimamisha kazi afisa mkuu wa hospitali ya rufaa ya Kenyatta Lily Koros kufuatia sakata ya upasuaji wa kimakosa iliyotokea hospitalini humo. Baadhi ya wabunge sasa wanasema tayari wamekusanya saini 100 kuhakikisha wanamtimua waziri Kariuki.