19th February, 2018
Waziri wa usalama wa kitaifa Fred Matiang’i amezuru eneo tete la Kerio Valley ambako kumeendelea kushuhudiwa uvamizi wa mifugo. Wakati wa ziara hiyo, waziri Matiang'i amezitaka shule zote zilizofungwa kufunguliwa huku akiviagiza vitengo vya usalama kutoa ulinzi kwa shule zote. Matiangi ameteua kikosi maalum cha maafisa wa kukabiliana na wahalifu na kuwaamrisha wakuu wa usalama kuwa macho.