.
12th February, 2018
Idara ya jeshi imetoa hakikisho kwa umma kwamba uteuzi wa makurutu utafanyika pasina ulaghai wala visa vyovyote vya ulaji rushwa. Naibu wa mkuu wa majeshi, Joseph Kasaon amesema shughuli hiyo iliyoanza rasmi hii leo itaendelea kwa mwezi mzima, lengo likiwa kuwateua makurutu elfu mbili kati yao mia mbili wakiwa wa jinsia ya kike.