12th February, 2018
Wakili Harun Ndubi alishtakiwa kwa kuendesha gari akiwa mlevi. Ndubi ambaye alikamatwa jana usiku karibu na makao ya Ikulu, alifikishwa katika mahakama ya Milimani na kusomewa mashtaka dhidi yake, ambapo polisi wanamshtaki kwa kutumia kileo na kisha kuendesha gari na kukataa kupuliza kifaa cha alco blow walipomtaka afanye hivyo. Aliachaliwa kwa dhamana ya shilingi elfu thelathini. Kesi hiyo itasikizwa Februari tarehe ishirini na tatu mwezi huu.