31st January, 2018
Jioni hii na kwa siku ya pili sasa, Wakenya watasalia kukosa matangazo kutoka kwa runinga za KTN News, NTV na Citizen TV baada ya serikali kutangaza kuwa televisheni hizo zitasalia kufungwa hadi uchunguzi wanaofanya utakapokamilika. Waziri wa usalama wa kitaifa dkt Fred Matiang’i anasema sababu ya kufungwa kwa televisheni hizi ni kutokana na vyombo hivyo kukaidi agizo la serikali kuwataka kutoshiriki kile anasema ni kuchochea uapisho haramu. Matiang’i aidha amesema kuwa uchunguzi umeanzisha kuhusiana na uapisho wa raila odinga hapo jana katika bustani ya Uhuru park akisisitiza hafla hiyo ni haramu. Hapo jana, waziri matiang'i aliratibu kwenye gazeti rasmi la serikali kuwa vuguvugu la nrm chini ya muungano wa NASA ni kundi haramu.