28th January, 2018
Biwi la simanzi limetanda katika kijiji cha Kawese kaunti ya
Kisumu west wakati wa mazishi ya jamaa watano wa familia
moja waliofariki kwenye ajali katika eneo la salgaa kwenye
barabara ya nakuru – Eldoret.Martin Odol na
wanawe wanne walifariki mkesha wa mwaka mpya baada ya
kuhusika kwenye ajali hiyo ambayo pia ilisababisha maafa ya
jumla ya watu 36. Na hii leo, wakaazi wamefika kwenye boma
la familia hiyo kuwapa mkono wa buriani . Kwa mujibu wa
familia hiyo mazishi haya yalicheleweshwa ili kutoa nafasi
kwa mkewe odol aliyekuwa hospitalini kupata nafuu ili
kuweza kushiriki mazishi hayo