×
× KTN KTN News KTN Morning Express KTN Leo Leo Mashinani The Big Story Checkpoint News Center E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian Entertainment Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified Jobs Games Crosswords Sudoku The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login
×
Show Swahili

Mipango ya Mazishi:Mazishi ya mwendazake Yvonne Wamalwa kufanyika Jumamosi

27th January, 2018

Yvonne Nambia Wamalwa, mkewe aliyekuwa makamu wa rais marehemu Michael Kijana Wamalwa, atazikwa Jumamosi wiki ijayo kwenye shamba lake la milimani mjini Kitale, kaunti ya Trans Nzoia. Mwenyekiti wa kamati ya mazishi Musikari Kombo amesema kwamba ibaada ya wafu itafanyika siku ya alhamisi katika kanisa katoliki la Consolata Shrine, eneo la Westlands, jijini Nairobi.  Baadaye mwili wa marehemu utapelekwa nyumbani kwake mtaa wa Karen, Nairobi, usiku kucha kabla ya kusafirishwa kitale siku ya ijumaa.  Jamaa na marafiki wanaendelea kukusanyika katika mtaa wa karen mipango ya mazishi inapoendelea.  Yvonne alifariki siku ya alhamisi katika hospitali ya Nayuki Cottage alikokuwa amekimbizwa kupokea matibabu.  Mwili wa mwendazake umehifadhiwa katika chumba cha maiti cha Lee.  Viongozi kadha wanazidi kutoa rambi rambi zao kwa familia ya Wamalwa.

.
RELATED VIDEOS