.
24th January, 2018
Baadhi ya waakilishi wa wadi wa kaunti ya Nairobi wamejitokeza kumtetea seneta Johnston Sakaja kufuatia tuhuma zilizotolewa na mbunge wa Gatundu South Moses Kuria kuwa anashirikiana kwa karibu na upande wa upinzani. Taarifa hii imetolewa mapema leo kurejelea hatua ya Sakaja kusaidia kutolewa jela kwa mbunge wa NASA Babu Owino.