×
× KTN KTN News KTN Morning Express KTN Leo Leo Mashinani The Big Story Checkpoint News Center E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian Entertainment Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified Jobs Games Crosswords Sudoku The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login
×
Show Swahili

Mwanamuziki wa jazz nchini Afrika Kusini Hugh Masekela ameaga dunia

23rd January, 2018

Mwanamuziki  wa jazz nchini Afrika Kusini Hugh Masekela ameaga dunia. Mwanamuziki huyo ambaye ni gwiji  wa utunzi, uimbaji na upulizaji wa tarumbeta inayofanana na mdomo bata, alifariki mapema leo jijini Johannesburg akiwa na umri wa miaka sabini na minane. Msanii huyo alijitosa kwenye fani ya uimbaji na burudani akiwa na umri mchanga wa miaka kumi na minne na kuvuma hadi kupata umaarufu jijini Johannesburg miaka ya 1950. Tungo zake nyingi zilikuwa zenye maudhui ya kutafuta usawa kwa mnyonge enzi za utawala wa makaburu wa Afrika Kusini. Mnamo oktoba mwaka uliopita, masekelo alitoa taarifa kwamba alikuwa anaugua saratani ya korodani au prostate cancer. Risala za rambirambi kutoka kwa mashabiki wake kote ulimwenguni zimeendelea kutapakaa kote kwenye mitandao.

.
RELATED VIDEOS