22nd January, 2018
Wanawake kutoka mashirika yasiyo ya kiserikali leo wameafanya maandamano wakitoa shinikizo kwa Rais Uhuru Kenyatta kuwateua mawaziri tisa wa kike kwa lengo la kuafikia usawa wa kijinsia nchini.Wanawake hao wanasema kuwa wakati umefika kwa serikali kuzingatia kuafikiwa kwa thuluthi mbili ya jinsia kama inavyohitajika kikatiba.