.
20th January, 2018
Edith Nyenze ambaye ni mke wa aliyekuwa mbunge wa kitui
magharibi, Francis Nyenze, hii leo amekabidhiwa cheti cha
kuwania kiti cha eneo bunge hilo kwa tikiti ya chama cha
wiper.Mpinzani wa Edith Nyenze kwenye uchaguzi wa
mchujo wa chama cha Wiper katika eneo bunge hilo, Maluki
Kitili Mwendwa alikuwepo na kuahidi kumuunga mkono edith
nyenze.