Wabunge wa Kike KNH:Walitaka kujua ukweli wa madai
20th January, 2018
Huku idara ya upelelezi nchini ikiarifiwa kuhusu madai ya
ubakaji hospitali ya Kenyatta, kina mama wabunge nchini
wamefanya ziara ya kutathmini hali ya mambo. Haya yanajiri
wakati taarifa kuhusu masaibu ya kina mama zikizidi kuwa
gumzo la kitaifa.