15th January, 2018
Gavana wa Nairobi Mike Sonko amevunja kimya chake tangu kutangaza kujiuzulu kwa naibu wake Polycarp Igathe, sasa akisema atashirikiana na viongozi wengine kuendesha serikali yake. Akionekana kupuuza athari zozote kufuatia kujiuzulu kwa Igathe, Sonko aliyekuwa akizungumza mjini Mombasa amesema bado anashauriana na chama cha cha Jubilee pamoja na wadau wengine kabla ya kutoa mustakabali wake.