Ubunifu mpya kuhusu teknolojia ya mifugo

KTN Leo | Wednesday 10 Jan 2018 7:10 pm

Jamii za wafugaji nchini zina kila sababu ya kutabasamu kufuatia ubunifu mpya utakao sajili na kuweka rekodi ya mifugo wao kwenye mitambo. Mfumo huu ambao unaongozwa na muungano wa madakatari wa mifugo nchini Kenya, unahusisha kuwaweka mifugo hawa vibano kwenye masikio, vibano vyenye nambari na ambavyo vinaweza kutambulika kwa njia ya electroniki.