28th December, 2017
Kinara wa NASA na kiongozi wa chama cha Wiper kalonzo musyoka amesema kuwa ni jukumu la rais Uhuru Kenyatta kuongoza mazungumzo ya kuleta maelewano kati ya serikali na upinzani, la sivyo viongozi wa NASA wataapishwa katika mojawapo ya harakati za kupigania haki yao. Kalonzo alikuwa kwenye hafla ya kuifariji familia ya aliyekuwa mbunge wa kitui magharibi Francis Nyenze. Kalonzo amesisitiza kuwa yeye pamoja na kinara wa NASA Raila Odinga waliibuka washindi kwenye uchaguzi wa Agosti nane na kuwa walipokonywa ushindi.