27th December, 2017
Viongozi wanne wa Jubilee akiwemo mbunge wa nandi hills Alfred Keter sasa wamepata afueni kwenye utata uliosababisha kufurushwa kwao kwenye kamati za bunge baada ya kukaidi msimamo wa chama cha jubilee. Keter pamoja na wabunge Silas Tiren, James Gakuya na Kangogo Bowen wamemshtaki kiongozi wa wengi aden duale, spika wa bunge justin muturi na kiranja wa wengi benjamin washiali kuhusiana na hatua hiyo wanayosema imekiuka haki zao.