Mabingwa wa Olimpiki Eliud Kipchoge na Vivian Cheruiyot watunukiwa tuzo
8th December, 2016
Mabingwa wa Olimpiki Eliud Kipchoge na Vivian Cheruiyot wametunukiwa tuzo za wanariadha bora wa mwaka huu nchini. Wawili hao ni miongoni mwa wanariadha waliotuzwa katika hafla maalum iliyoandaliwa hapo jana mjini Nairobi.