7th December, 2016
Viongozi wa eneo la North Rift wanajiandaa kumpokea rais Uhuru Kenyatta kwenye ziara yake inayotazamiwa kuanza eneo hilo hapo kesho. Rais Kenyatta aliyepangiwa kuandamana na naibu wake William Ruto, watazindua mradi wa ujenzi wa barabara ya kuunganisha kaunti za Uasin Gishu, Nandi na Kisumu.